Kuna sababu anuai zinazomfanya mwanamke amsaliti mumewe. Ni
muhimu kutambua kuwa mwanaume ni kiumbe mwenye hisia kali na daima ahisi raha
na amani. Baadhi ya nyakati hufanya usaliti ili kuziba pengo la upungufu
unaotokea katika maisha yake. Zifuatazo ni sababu kubwa ambazo zinamfanya
amsaliti mumewe:
1. KUTOMPA KIPAUMBELE
NA KUTOMTHAMINI
Tunatambua kuwa mke anafanya kazi kubwa sana ambayo lau kama
ingekuwa ni kampuni basi pangehitajika watu zaidi ya 10 kuzifanya... atamtunza
mume, watoto, nyumba na familia kwa ujumla...
Wakati fulani mume anaweza akampuuza na asimthamini, licha ya
kujitoa kwa moyo wote kumtunza na kuihudumia familia... Hivyo, kutotoa
kipaumble kwa mke ni kosa kubwa ambalo linaweza likamgharimu mume... mke
akipata mtu anayempa kipaumbele na kumuonesha thamani hakika hataacha kuitumia
hiyo fursa.
2. UKOSEFU WA MAHABA
Kwa asili mwanamke ana silika ya hitajio la kupendwa... Mwanamke
anahitaji kupendwa... mwanaume yeye ana silika ya kupenda ngono... ukimpa ngono
tu basi, anaridhika... mwanamke anahitaji kuengaengwa, anahitaji kudekezwa,
anahitaji aambiwe maneno yenye ladha adimu yaliyochanganywa na vionjo vya
ndimu... mwanamke anataka hivyo.. anataka aone kama anapendwa... anataka aone
mtu anamwambia vile alivyo, alivyo maridhawa, amueleze hisia zake... ampe lugha
ya kimajnun... mwanamke anamtaka Majnun... sasa akimpata mtu wa aina hiyo,
tofauti na mumewe, huwa ni balaa tupu... mnanipata hapo?
![]() |
KUMBATIA PENZI LA KWELI. |
3. USALITI WA MUME
Miongoni mwa mambo ambayo huibadilisha roho ya mwanamke ni pale
anapogundua kuwa mumewe kipenzi anamsaliti... Hapo mwanamke anaweza akabadilika
kabisa... Wapo wanaosamehe, lakini wapo wanaolipiza kisasi...
4. KUTOJIAMINI
Mwanamke anahitaji mwanaume anayemfanya ajiamini... iwapo mumewe
hatekelezi jukumu hilo, akimpata mtu anayemfanya ajiamini, yanaweza kutokea
mengine kabisa... Hivyo, nasaha zangu kwa kaka zangu kuyaangalia kwa makini
mambo haya...
Imeandaliwa na Sharrif Kisuda mwanasaikolojia na mshauri katika
mafanikio na mapenzi.
0 maoni:
Chapisha Maoni